Afisa wa umoja wa mataifa amesema watu 32 wamekufa jumatatu wakati ndege ya UN ilipoanguka katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.
Msemaji wa umoja wa mataifa Farhan Haq amesema mtu mmoja alinusurika katika ajali iliyotokea wakati ndege ikijaribu kutua kwenye mji mkuu wa Congo , Kinshasa.
Maafisa wa usalama wanasema mvua ilikuwa ikinyesha katika eneo hilo wakati ndege ilipogonga kwenye njia zake na kupasuka vipande vipande.
Ndege hiyo ilikuwa inatokea kaskazinimashariki mwa mji wa Kisangani.
Balozi wa marekani katika umoja wa mataifa Susan Rice alisema amesikitishwa sana kuhusiana na ajali hiyo. Amesema kupoteza maisha kwa wafanyakazi wa masuala ya kibinadamu na walinda amani wa umoja wa mataifa ni pigo kwa UN na watu wa Congo.