Watu 11 wamepoteza maisha katika ajali mbaya ya basi la abiria na lori la mizigo iliyotokea Alhamisi, asubuhi mkoani Tanga, nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoani humo Hassan Hashim, majeruhi walipelekwa katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza ambapo wanapatiwa matibabu.
Hashim anasema ajali hiyo ilitokea kutokana na dereva wa lori kutokuwa makini wakati alipoamua kupita gari lingine na kwenda kuligonga basi hilo usoni linalo milikiwa na kampuni ya Simba Mtoto.
Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni madereva wote wa lori na basi hilo lililokuwa likutokea mkoani Tanga na kuelekea jijini Dar es salaam.
Mpaka hivi sasa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa kuhusu hali ya majeruhi ama kama idadi ya vifo imeongezeka.