Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 03:14

Ajali ya basi likielekea Afrika kusini limeua watu 10 na wengine 35 kujeruhiwa


Jimbo la Limpopo nchini Afrika kusini.
Jimbo la Limpopo nchini Afrika kusini.

Kulingana na mamlaka, dereva huyo alikuwa mgeni katika kazi yake na hakuwa anayafahamu  mazingira.

Basi lililokuwa likisafiri kutoka Zimbabwe lilipoteza udhibiti na kupinduka katika jimbo la Limpopo, kaskazini mashariki mwa Afrika kusini, na kuwaua watu 10 na kuwajeruhi wengine 35, wizara ya usafiri nchini humo imesema leo Jumatano.

Wanaume watano na wanawake watano, ambao wanaoripotiwa ni raia wa kigeni, walikuwa njiani kuelekea Johannesburg wakati ajali hiyo ilipotokea Jumanne usiku, serikali imesema katika taarifa. Gari lilipita juu ya mzunguko likiwa katika mwendo wa kasi, na kupoteza udhibiti na kupinduka, kuua na kujeruhi abiria wake katika ajali hiyo, taarifa ilisema.

Kulingana na mamlaka, dereva huyo alikuwa mgeni katika kazi yake, na hakuwa anayafahamu mazingira. Abiria waliojeruhiwa walipelekwa katika hospitali za eneo hilo.

Afrika Kusini ina moja ya mitandao ya barabara iliyoendelea zaidi barani Afrika lakini pia ipo katika rekodi mbaya sana ya usalama barabarani, kwa kiasi kutokana na kuendesha gari kizembe na magari yasiyo na viwango vya kutembea barabarani.

Katika ajali mbaya zaidi ya barabarani nchini Afrika Kusini mwaka huu, watu 45 walikufa wakati wakielekea kwenye hafla ya kidini mwezi Machi wakati basi lao lilipotumbukia kwenye daraja kaskazini mwa nchi hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG