Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 27, 2024 Local time: 08:51

Ajali ya barabarani yaua watu saba Kenya


Barabara Kuu ya Nairobi-Mombasa nchini Kenya
Barabara Kuu ya Nairobi-Mombasa nchini Kenya

Watu saba wamepoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha basi dogo la abiria na lori katika eneo la Sultan Hamud huko Kaunti ya Machakos.

Lori hilo liligongana na gari dogo aina ya hearse ambalo lilikuwa linasafirisha wafiwa madakika kadhaa baada ya saa nne asubuhi huko eneo la Kalimbini liliyoko katika Barabara Kuu ya Nairobi -Mombasa, Jumamosi.

Lorri hilo liligongana uso kwa uso na gari hiyo iliyokuwa imebeba wafiwa. Kamishna wa polisi wa Kaunti ya Makueni Maalim Mohammed amethibitisha ajali hiyo mbaya na kusema kuwa huenda idadi ya vifo ikaongezeka.

Ripoti za ajali barabarani zinaeleza kuwa katika mwezi huu wa kusheherekea Krismas, Disemba, ambao haujamalizika, tayari idadi ya waliokufa katika ajali ya barabarani imeongezeka kuwa mara mbili ya zile ajali zilizotokea miezi 11 iliyopita.

Siku ya Jumatatu Disemba 11, watu 19 walipoteza maisha katika ajali mbaya iliyotokea kwenye Daraja la Kamukuywa katika barabara ya Webuye-Kitale.

Siku iliyofuatia, zaidi ya watu 30 waliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika tukio jingine la ajali lililohusisha basi la Modern Coast na magari mengine 13 katika eneo la Sachagwan kwenye barabara kuu hiyo.

Ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa lori ambaye alikuwa anafukuzwa na Mamlaka ya Uchukuzi na Usalama Kenya (NTSA) aliposhindwa kuidhibiti gari na kugongana na magari kadhaa yaliyokuwa yanakuja mbele yake ikiwemo Basi ya Modern Coast, Matatu nne aina ya Nissan, lori na magari binafsi madogo kadhaa ikisababisha vifo.

Hata hivyo NTSA imesema kuwa matukio yote hayo ya ajali yalitokana na uzembe wa madereva na makosa ya kibinadamu.

Serikali kupitia Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’l na Waziri James Macharia wameahidi kumaliza wendawazimu katika barabara za Kenya kwa kuwalenga polisi wa barabarani, shule zinazofundisha udereva na madereva wazembe kuhakikisha wanatimiza wajibu wao.

XS
SM
MD
LG