Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Novemba 28, 2024 Local time: 10:38

Ahukumiwa miaka 25 gerezani kwa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994


Mahakama ya Brussels, Jumatatu imemuhukumu mwanamume wa miaka 65 raia wa Ubelgiji na Rwanda kifungo cha miaka 25 gerezani kwa mauaji na ubakaji uliofanywa wakati wa mauaji ya kimbari ya Rwanda ya 1994.

Emmanuel Nkunduwimye, alikutwa na hatia ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki pamoja na ubakaji wa mwanamke wa Kitutsi.

Nkunduwimye, ambaye alikamatwa kwa mara ya kwanza Ubelgiji, 2011, alikuwa mmiliki wa gereji katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali, Aprili 1994 wakati mauaji ya kimbari yalipoanza.

Gereji yake ilikuwa sehemu ya majengo mengi yaliyokuwa eneo la mauaji yaliyofanywa na wanamgambo wa Interahamwe.

Nkunduwimye alikuwa karibu na viongozi kadhaa wa wanamgambo akiwemo Georges Rutaganda, ambaye alihukumiwa kifungo cha maisha na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ya Rwanda na kufariki dunia 2010.

Forum

XS
SM
MD
LG