Mahakama katika mji wa kusini wa Huye ilimtia hatiani Beatrice Munyenyezi, mwenye umri wa miaka 54 kwa mashtaka ya uhalifu wa mauaji ya kimbari katika kushiriki, kuchochea kutekelezwa mauaji na kushiriki ubakaji.
Hata hivyo hakutiwa hatiani kwa mashaitaka ya kupanga mauaji ya kimbari, gazeti la kitaifa la Rwanda limeandika.
Hukumu hiyo imefanyika siku chache baada ya Rwanda, kuadhimisha miaka 30 ya mauaji hayo ya Aprili mpaka Julai 1994, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 800,000, wengi wao wakiwa ni Watutsi, lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Forum