“Ofisi ya rais inataka kufafanua kuwa Afrika Kusini bado inatii mkataba wa Roma. Ufafanuzi huu unafuatia makosa katika kauli zilizotolewa wakati wa mkutano na vyombo vya habari ulioendeshwa na chama tawala cha African National Congress (ANC), “ ofisi ya Ramaphosa ilisema katika taarifa ya Jumanne usiku.
Ramaphosa mapema Jumanne aliuambia mkutano wa vyombo vya habari kwamba chama chake cha ANC kimeamua Afrika Kusini ijiondowe katika mahakama ya ICC, ambayo mwezi uliopita ilitoa hati ya kumkamata Rais wa Russia Vladimir Putin.
Hati ya ICC ilimaanisha kuwa Pretoria, ambayo itakuwa mwenyeji wa mkutano wa nchi wanachama wa BRICS mwaka huu ambazo ni Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini, italazimika kumkamata Putin atakapowasili kushiriki mkutano huo.