Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 19:42

Afrika Kusini yarejesha masharti ya kutotoka nje usiku, yapiga marufuku uuzaji pombe


Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alitangaza Jumapili kwamba serikali yake inarejesha masharti yaliyokuwepo ya kutotoka nje usiku na kupiga marufuku uuzaji wa pombe.

Alisema anachukua hatua hiyo katika juhudi za kupunguza misongamano ya majeruhi, inayoshuhudiwa kwenye mahospitali, hali ambayo inawanyima nafasi za matibabu watu wenye maambukizi ya virusi vya Corona, ambao wameendelea kuongezeka kila uchao.

"Hivi ni vita vya kuokoa maisha na tunahitaji kila kitanda katika hospitali zetu," alisema Ramaphosa.

Katika siku za karibuni kumekuwa ripoti za vituo vya afya kukumbwa na misongamano mikuwa na uhaba wa vifaa vya kitabibu, hali ambayo serikali imedai inachangiwa kwa kiasi kikubwa na ajali zinazosababisha na ulevi.

Wakati huo huo, kufuatia kulegezwa kwa baadhi ya masharti ya kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona, maambukizi yameongezeka kwa kasi katika maeneo mabalimbali nchini humo.

Utawala wa Ramaphosa ulikuwa umeweka masharti makali Zaidi duniani mnamo mwezi Machi, hatua ambayo ilichangia kupungua kwa kasi ya maambukizi.

Hata hivyo, baadaye rais huyo alitangaza kulegezwa kwa baadhi ya masharti, kufuatia hofu kubwa ya kudhoofika kabisa kwa uchumi wa taifa hilo la Kusini mwa Afrika, ambao tayari ulikuwa ukisuissua hata kabla ya kutokea kwa janga la Corona.

Akilihutubia taifa kupitia vyombo vya habari, Ramaphosa alisema kwamba wanasayansi wanakadiria kuwa kati ya watu 40,00 na 50000, huenda wakafa kufikia mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa mujibu wa takwimu za Shirka la Afya Duniani, WHO, Afrika Kusini ndiyo nchi yenye idadi kubwa Zaidi ya maambukizi barani Afrika, na ni ya nne duniani, kwa nchi zenye idadi kubwa Zaidi ya maambukizi ya kila siku.

Ramaphosa alisema marufuku hiyo ya kutoka nje usiku itaanza kutekelezwa Jumatatu tarehe 12 mwezi Julai, 2020, na itakuwa ikianza saa tatu usiku hadi saa kumi asubuhi kila siku.

XS
SM
MD
LG