Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 01:29

Jaji: Kumfutia mashtaka Rais Zuma haukuwa uamuzi wa busara


Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma akiongea kwenye mkutano wa kuadhimisha siku ya haki za binadamu huko Durban, Afrika Kusini.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma akiongea kwenye mkutano wa kuadhimisha siku ya haki za binadamu huko Durban, Afrika Kusini.

Jaji katika mahakama moja nchini Afrika Kusini amesema leo Ijumaa kwamba uamuzi wa mahakama wa mwaka 2009 wa kufuta mashtaka ya rushwa takribani 800 dhidi ya Rais Jacob Zuma ulikuwa sio wa busara na alitoa wito kwa mashtaka hayo kuchunguzwa tena.

"Uamuzi wa kutoendelea na mashtaka dhidi ya bwana Zuma ni uamuzi usio sahihi na unatakiwa kutathminiwa," alisema jaji wa mahakama kuu ya Pretoria, Aubrey Ledwaba.

Bwana Zuma anatakiwa kukabiliwa na mashtaka hayo kama yalivyo. Awali mahakama ilitoa uamuzi huo kulingana na maelezo ya kuingilia kati ya simu na yaliwasilishwa na timu ya utetezi ya bwana Zuma. Walisema mashtaka ya mwishoni mwa mwaka 2007 huwenda yakawa sehemu ya mpango wa kisiasa dhidi ya Zuma, na uamuzi wa mahakama kutoendelea na mashtaka hayo ulimruhusu Zuma kuendelea kuwania urais.

XS
SM
MD
LG