Uuzaji na ununuzi wa huduma za ngono hautachukuliwa tena kama uhalifu chini ya sheria iliyopendekezwa na wizara ya sheria.
Kulingana na makundi yanayotetea sheria hiyo, kuna zaidi ya wafanyabiashara wa ngono 150,000 nchini humo.
Waziri wa sheria Ronald Lamola ameuambia mkutano wa waandishi wa habari “Inatarajiwa kuwa kuhalalisha biashara hiyo kutapunguza ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya wafanyabiashara wa ngono.”
Afrika Kusini ni moja ya nchi yenye visa vingi vya ukimwi duniani na imekumbwa na ongezeko la wimbi la ukatili dhidi ya wanawake.