Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:39

Afrika kusini inachunguza ripoti ya wanajeshi wake waliwatesa raia DRC


Baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Congo
Baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Congo

Jeshi la Afrika kusini limeanzisha uchunguzi kuhusiana na ripoti kwamba wanajeshi wake 1,000 katika kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC waliwashambulia na kuwatesa wanavijiji.

Taarifa ya jeshi ilisema hatua za adhabu zitachukuliwa ikiwa ripoti ambazo zinasemekana zimewasilishwa na raia ni za ukweli. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema Jumatatu kwamba Ofisi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Congo-MONUSCO imepokea malalamiko manne ya unyanyasaji ikijumuisha shutma tatu za kadhia ya ngono inayowajumuisha waathirika watu wazima. Tuhuma ya nne inahusiana na kupigwa kwa mvulana mwenye umri wa miaka 17 huko mashariki mwa jimbo la Kasai na walinda amani hao.

Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa
Stephane Dujarric, msemaji wa Umoja wa Mataifa

Dujarric anasema muathirika huyo alifikishwa mbele yao na shirika la kuhudumia watoto katika Umoja wa Mataifa-UNICEF. Aliongeza kusema kwamba Umoja wa Mataifa uliomba uchunguzi unaofanywa na Afrika kusini ukamilike ndani ya muda wa siku 90.

XS
SM
MD
LG