Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:56

Africa yaendeleza mkakati wa kutotegemea wahisani


Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat
Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat

Tume ya mawaziri kumi wa fedha wanaowakilisha kanda tano za bara la Afrika wamepongeza hatua iliyofikiwa na mataifa ya Kiafrika ya kuendelea kukusanya nguvu kwa ajili ya kujiendeshea mambo yake bila kusubiri tena misaada ya wahisani.

Mawaziri hao kumi wa fedha wameeleza hayo mjini Kigali mwishoni mwa juma walipokutana kutathmini mafanikio ya mkakati huo uliochukuliwa na marais wa Afrika miaka miwili iliyopita.

Mwaka 2016 mwezi Julai ndipo marais wa kiafrika walipokutana Kigali Rwanda na kukubaliana kwamba kila nchi itenge asilimia sifuri nukta mbili kutokana na mapato ya baadhi zinazoingizwa kwenye nchi hiyo kutoka ng’ambo.

Umoja wa Afrika umesema unaachana na kutegemea misaada ya wahisani kwa ajili ya kuendesha mambo yake.

Umesema kuwa ilibainika kuwa zaidi ya asilimia 80% ya bajeti inayotumiwa na kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) ilitegemea pesa za wahisani.

Miaka miwili baadaye mwenyekiti wa kamisheni ya umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ametoa taswira ya jinsi mataifa hayo ya Kiafrika yanavyoendelea kuchangia kiasi hicho cha mapato kama ilivyokubaliwa na wakuu wa nchi hizo.

"Mataifa 12 yanaendelea na kasi kubwa ya kutenga kiasi hicho kulingana na kiwango kilichokuliwa. Hii ina maana ndani ya muda wa miaka miwili tunakaribia kufikiwa kiwango cha msingi kinachotakiwa," amesema.

Viongozi wa kiafrika kwa nyakati tofauti wametaja kwamba kuendelea kutegemea mataifa wahisani kwa ajili ya kuendeshea mamo yake siyo tu kwamba yanadumaza maendeleo ya bara hilo, lakini pia hii inatoa mwanya wa kuendelea kuwepo kwa ukoloni mambo leo kutoka mataifa makubwa.

Waziri wa fedha wa Rwanda Balozi Claver Gatete amesema mataifa yote ya Kiafrika yataweza kutoa mchango huo kwenye kamisheni ya umoja huo.

Anaeleza kuwa: "Michango hii itaufanya umoja wa Afrika kujitosheleza kwa kiwango cha asilimia 100% ktk kutekeleza mahitaji ya bajeti yake,ikiwa ni pamoja na asilimia 75% kuwekwa kwenye kuendesha miradi mikuwa ya bara hili huku asilimia 25% ikiwekwa kwenye masuala ya ulinzi na usalama.

Sisi hapa kama mawaziri wa fedha hatutachukua nafasi kujadili yale yaliyopitishwa na marais wetu, la hasha tunachokifanya hapa ni kujadiliana utekelezwaji wake."

Hadi mwezi Disemba 2017 kwa ujumla mataifa 21 ya bara la Afrika ndiyo yalikuwa yamekwisha anza kutoa michango hiyo japo kwa viwango tofauti.

Kadhalika mawaziri wa fedha Nigeria, Morocco na Cameroon nao walihudhuria kama wanatume japo awali hawakuwa sehemu ya tume hiyo.

XS
SM
MD
LG