Wasomi kutoka kote barani Africa walikutana mjini Johanesburg wiki ilopita katika mkutano wa vyuo vikuu vya Kiafrika.Hii ikiwa ni sehemu ya kujadili baadhi ya masuala makubwa yanoyokabili masomo ya juu barani Africa hivi leo.
Wasomi wanasema kuwa vyuo vikuu ni ufunguo wa maendeleo kwa Africa.
Lakini wasomi wa kiafrica wanasema kuwa kutoka Cape hadi Cairo, kuna ukosefu wa ufadhili, miundo mbinu mibaya na mahitaji yanafanya kuelimisha wanafunzi wa Afrika kuwa changa moto kubwa.
David Mfinanga ni kansela msaidizi kutoka chuo kikuu cha dar es salaam anasema, nchi nyingi zinajaribu kuzidisha idadi ya wanafunzi wanaohitimu kwa sababu ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi. Lakini raslimali ni haba, kwa hiyo hilolinaathiri ubora vilevile na hivyo tunahangaika kusawazisha hayo masuala mawili kwa sababu unahitaji idadi, unahitaji wanafunzi Zaidi, lakini pia unahitaji kuendeleza ubora, lakini rasli mali ni chache .
Na katika mojawapo ya vyuo vikuu vikubwa huko kusini mwa Africa, fedha ndio tatizo linaloendelea.
Hivi karibuni chuo kikuu cha Johannesburg kilifanya mkutano kwa ajili ya kuboresha elimu ya juu afrika.
David Mfinanga kutoka chuo kikuu cha Daresalam anasema kutetea kuwepo kwa elimu ya juu kunaweza kuwa mapambano makali kwa bara ambalo mara nyingi linakabiliwa na matatizo makubwa Zaidi kama vile vita, njaa na umasikini.
Lakini anasema kiwango bora Zaidi cha masomo ya chuo kikuu ndio suluhisho kwa mengi ya matatizo haya.
Hata hivyo wataalam wanasema seriklai pia zinahitaji kuangalia kwa undani jinsi ya kuendeleza wahitimu.
Hakuna matatizo ambayo yatasuluhishwa kwa usiku mmoja, mataizo yanahitaji uwekezaji mkubwa, na ahadi za serikali na juhudi za pamoja za kila mtu anayehusika.
Lakini wanasema, hili halifanyi tatizo hili kuwa na umuhimu kidogo. Mustakbal wa Africa unategemea hili.