Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 14:50

Shambulizi lauwa watu 30 Afghanistan


Wanamgambo wa Taliban wanaendelea kuwadhuru raia nchini Afghanistan. Septemba 2015.
Wanamgambo wa Taliban wanaendelea kuwadhuru raia nchini Afghanistan. Septemba 2015.

Kundi la kigaidi la Taliban muda mfupi baadae wamedai kuhusika na shambulizi hilo.

Maafisa wa Afghanistan wamesema mabomu mawili ya kujitoa mhanga yameuwa zaidi ya watu 30 na kujeruhi wengine zaidi ya 80 Jumatano .

Walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa washambuliaji waliulenga msafara wa magari uliokuwa ukitoka kwenye majengo ya bunge.

Baadhi ya walioathiriwa ni maafisa wa usalama wa ngazi ya juu, raia wa kawaida pamoja na wabunge. Ripoti zinasema mshambuliaji mmoja wa kujitoa mhanga alijilipua karibu na ofisi za bunge kwenye mtaa wa Darulaman kabla ya mwenzake kujilipua akiwa kwenye gari lililojaa vilipuzi muda mfupi baadae.

Kundi la kigaidi la Taliban muda mfupi baadae wamedai kuhusika na shambulizi hilo.

Kundi la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limekemea shambulizi hilo likisema kuwa kundi la Taliban halina huruma na maisha ya binadamu, na wameomba uchunguzi huru ufanyike kuwafikisha wahusika mbele ya sheria.

XS
SM
MD
LG