Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 06:30

Mbunge Adam Schiff adai Trump amefanya makosa


Mwenyekiti wa kamati ya Ujasusi na Usalama Adam Schiff.
Mwenyekiti wa kamati ya Ujasusi na Usalama Adam Schiff.

Schiff anasema hatua za Trump kabla na baada ya uchaguzi zinathibitisha amefanya makosa

Mbunge mdemokrat Adam Schiff alilinda kwa nguvu zake zote kuendelea kwa uchunguzi wa kamati yake juu ya mafungamano ya rais Trump na Russia kati kati ya madai kutoka kwa rais wa Marekani na warepublikan wengine kwamba mbunge huyo ajiuzulu uenyekiti wa kamati hiyo.

Schiff ni mwenyekiti wa kamati yenye nguvu ya masuala ya Ujasusi na Usalama. Licha ya ripoti ya mwendesha mashitaka mkuu William Barr kusema kwamba ripoti ya Mueller inamwondolea Trump tuhuma za kwamba kampeni yake imeshirikiana na Russia , Schiff anasema hatua za Trump kabla na baada ya uchaguzi zinathibitisha kwamba amefanya makosa.

“Nafikiri ni kukosa heshima,nafikiri ni kukosa kufuata taratibu nafikiri ni kukosa uzalendo na ndio nafikiri ni ufisadi" mbunge huyo alisema katika ufunguzi wa kikao cha kamati yake Alhamisi.

Imetayarishwa na Sunday Shomari

XS
SM
MD
LG