Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 19:16

Operesheni "rudi nyumbani" Kenya yaingia dosari


Hali ya wasiwasi imejitokeza katika eneo la Rift Valley nchini Kenya kufuatia uvamizi ambapo watu wawili waliuwawa huko Kuresoi siku moja tu kabla ya mwendesha mashitaka wa Mahakama ya Kimataifa Luis Moreno Ocampo kuwasili nchini Kenya.

Watu hao wawili waliuwawa kwa kukatwa katwa na mapanga na watu wasiojulikana lakini duru zinasema mauaji hayo yametokea baada ya vitisho dhidi ya wakimbizi kutolewa na kundi la watu wenye uhusiano wa karibu na baadhi ya washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi ambao wanakabiliwa na tishio la kupelekwa mbele ya mahakama ya uhalifu wa kimataifa (ICC) huko nchini Uholanzi.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika Mwangi Geita anaripoti kuwa mamia ya watu ambao walikuwa wamerudi makwao kufuatia mpango wa serikali wa “operesheni rudi nyumbani” sasa wameanza kutoroka na kurejea kwenye makambi ya muda kufuatia tukio hilo, vitisho vya kuzuka kwa ghasia mpya na kuzorota kwa hali ya usalama kwa ujumla.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG