Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:37

Washirika wa Ingabire wakamatwa


Washirika wa Ingabire wakamatwa
Washirika wa Ingabire wakamatwa

<!-- IMAGE -->

Maafisa wa Rwanda wamewakamata watu 3 wanaotuhumiwa ni waasi wa kihutu kwa shutuma za kushirikiana na kiongozi wa upinzani Victoire Ingabire. Wanasema watu hao watatu wamekuwa wakifanya kazi na Ingabire kuiyumbisha nchi.

Siku ya Jumatano, maafisa wa Rwanda walimkamata Ingabire kwa madai kwamba anakana mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na kushirikiana na waasi wa kihutu wa Rwanda waliopo Congo. Aliachiwa kwa dhamana jana.

Ingabire anaongoza chama kisichosajiliwa cha United Democratic Forces. Anatoa wito kwa wanachama wa jeshi la Rwanda na chama tawala kuchunguzwa kwa shutuma za uhalifu dhidi ya watu wenye asili ya kihutu wakati wa mauaji ya kimbari.

XS
SM
MD
LG