Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:55

Kampeni za mwisho za uchaguzi Sudan zapamba moto


Kampeni za mwisho za uchaguzi Sudan zapamba moto
Kampeni za mwisho za uchaguzi Sudan zapamba moto
<!-- IMAGE -->

Wanachama wa chama cha siasa huko Sudan waliandamana kwa ajili ya kupata uungaji mkono katika siku yao ya mwisho ya kampeni kabla ya kuanza kwa uchaguzi mkuu Jumapili.

Rais Omar Al Bashir alizungumza katika mkutano huko Dalgo kaskazini mwa Sudan ambapo aliapa kuendeleza miradi ya maendeleo nchi nzima.

Uchaguzi huo wa rais, bunge na kanda ni uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi tangu 1986.

Hata hivyo vyama kadhaa vya upinzani vilitangaza mipango ya kususia baadhi ya uchaguzi vikikishutumu chama tawala cha National Congress kwa kujiandaa kwa wizi wa matokeo.

XS
SM
MD
LG