Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:06

Majeshi na wapiganaji Somalia hawajali raia - Amnesty


Majeshi na wapiganaji Somalia hawajali raia - Amnesty
Majeshi na wapiganaji Somalia hawajali raia - Amnesty

Amnesty International inasema, makundi ya upinzani yenye silaha hufyetua mizinga na silaha nzito nzito kuelekea kambi za jeshi la serikali ya mpito, TFG na kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM.

<!-- IMAGE -->

Ripoti inasema majeshi ya serikali na ya AMISOM hujibu kwa mizinga na silaha kubwa kubwa na matokeo yake kunatokea majeruhi wengi kila wiki miongoni mwa raia. Benedicte goderiaux wa amnesty aliyetayarisha ripoti anasema, “tunaendelea kupokea ripoti kwamba serikali na majeshi ya AMISOM hayachukuwi tahadhari zinazohitajika kuhakikisha silaha zao haziwadhuru raia na makazi ya raia”.

AMISOM imeiambia Amnesty kwamba, haijibu mashambulio ya makundi yenye silaha kiholela kwa kushambulia maeneo ya raia. Serikali ya mpito nayo imesema haijaidhinisha mashambulio dhidi ya maeneo ya kiraia.

Wanajeshi kadhaa wa Umoja wa Afrika wanailinda serikali ya TFG ambayo hivi sasa inadhibiti sehemu ndogo tu ya mji mkuu wa Mogadishu. Marekani, Umoja wa Ulaya na baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki yamejitolea kutoa mafunzo kwa zaidi ya wanajeshi na polisi elfu 20 wa kisomali.

<!-- IMAGE -->

Goderiaux anasema ungaji mkono wa kimataifa kwa serikali ya mpito ni lazima lakini unabidi ufanyike kukiwepo na masharti. Anasema wanadhani jumuia ya kimataifa ni lazima isaidiye zaidi katika sauala la usalama na uwajibikaji wake. Wanadhani ni lazima jumuia ya kimataifa ihimize zaidi katika suala la uwajibikaji badala ya kutoa ungaji mkono bila ya kuuliza suali lolote.

Somalia imekumbwa na ghasia na mapigano baada ya kuanguka kwa utawala wa Said Barre 1991. Kulikuwepo na matumaini makubwa baada ya kuteuliwa kwa Sheik Sharif Ahmed kua rais wa serikali ya mpito na kuondoka kwa majeshi ya Ethopia kutoka nchi hiyo 2009. Lakini Alexander Ramsbotham mhariri wa jarida la Accord, linalochapisha juhudi za amani za kimataifa huko Uingereza anasema amani imekua ni ndoto kwa nchi hiyo.

“Mara kwa mara mnamo miongo miwili iliyopita majeshi ya kigeni na juhudi za kuikarabati taifa hilo zimeshindwa kuleta amani Somalia na anadhani juhudi za mwisho za serekali ya mpito zinakumbwa na matatizo sawa na hayo ya juhudi za zamani.”

Anasema sera ya kimataifa kuelekea Somalia inazingatia matatizo ya uharamia na kupambana na ugaidi na wala si kukabiliana na masuala ya usalama. Na anasema kuwalinda raia haiko juu kwenye ajenda hiyo.

XS
SM
MD
LG