Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 16:19

Wakenya Wataka majina 20 ICC yafichuliwe


Wananchi wengi wa Kenya wangependa kuona kuwa majini ya watu 20 yaliyowasilishwa katika mahakama ya ICC huko the Hague, Uholanzi, yanafichuliwa. Majina hayo inayosemekana kuwa na watu maarufu nchini Kenya yaliwasilishwa katika mahakama ya the Hague na mwendesha mashitaka mkuu wa ICC Luis Moreno Ocampo kwa madai kuwa walihusika katika kuchochea ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya mwaka 2007.

Katika mahojiano na Sauti ya Amerika mwenyekiti wa kamati ya maswala ya sheria ya bunge, Kenya, Paul Muite, alisema wakenya wengi wangependa kujua watu hao ni akina nani. Alisema mahakama iseme hadharani watu hao ni nani na kwamba uchunguzi uanzwe mara moja.

Mahakama hiyo sasa inatazamiwa kufanya uchunguzi wa kina dhidi ya watu hao na kupata uamuzi endapo wanafaa wafunguliwe mashitaka ama la.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG