Ajali ya mabasi mawili ya abiria katika mkoa wa Tanga nchini Tanzania Jumanne imesababisha vifo vya watu 22 na wengine zaidi ya 37 kujeruhiwa.
Ajali hiyo ilihusisha mabasi mawili kati ya basi la Mzuri lililokuwa linatokea mkoa wa Dar-Es-Salaam kuelekea Mombo, Korogwe, Hedaru mpaka maeneo ya Mazinde na basi lingine la Chatco likitokea Moshi-Arusha kuelekea Dae-Es-Salaam.
Wataalam wa usafirishaji Tanzania wanasema ajali za barabarani zinaendelea kutokea mara kwa mara nchini humo na kusababisha vifo vya watu wengi licha ya kuwepo mamlaka mbali mbali zinazosimamia usalama wa abiria na mali zao.
Sauti ya Amerika imezungumza na David Mziray, afisa habari wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu-SUMATRA nchini Tanzania, ambaye alielezea juhudi zinazofanywa na mamlaka yake kuhakikisha usalama wa abiria.