Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 06:27

Mapigano Mapya Somalia


Mapigano makali kati ya waasi wa Somalia na walinda amani wa Umoja wa Afrika yamewauwa watu 12 na kuwajeruhi zaidi ya 20 wengine.Mkuu wa kitengo cha magari ya kuhudumia wagonjwa huko Mogadishu alisema vifo hivyo vilijumuisha wanawake na watoto.

Mashahidi wanasema vifo vingi ni vya raia. Wakazi wanasema yalikuwa mapigano mabaya kuyaona katika miezi ya hivi karibuni. Wanasema mapigano yalianza mapema Ijumaa asubuhi.

Katika taarifa, kundi la wanamgambo la al-Shabab, lilisema lilishambulia vituo vya serikali na Umoja wa Afrika. Pande zote zilifyatuliana risasi na makombora karibu na makutano ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Makutano hayo yanajulikana kama K4 au kilomita nne. Eneo hilo linadhibitiwa na walinda amani, lakini limefanyiwa mashambulizi makali kutoka kwa wanamgambo. Walinda amani wanasema kudhibiti eneo la K4 ni muhimu ili kudhibiti mji.

Mapigano yametokea siku moja baada ya Umoja wa Mataifa kupiga kura ya pamoja kuongeza muda za shughuli za walinda amani wa Umoja wa Afrika katika nchi yenye mzozo wa vita kwa mwaka mmoja mwingine. Jeshi la AU huko Somalia lina wanajeshi wasiopungua 4,000 kutoka Uganda na Burundi.

XS
SM
MD
LG