Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 08:05

Obama anasema kimbunga kimepita


Rais Barack Obama amelihimiza Bunge la Marekani kuchukua hatua haraka katika baadhi ya vipaumbele vyake, kama vile mageuzi ya huduma za afya na uchumi, wakati alipokua anatoa hotuba yake ya kwanza juu ya hali ya taifa Jumatano usiku.

Akizungumza mbele ya mabaraza mawili ya bunge, Rais Obama alilihimiza bunge kumpelekea mswada juu ya kubuni ajira bila ya kuchelewa. Akitoa wito wa kuwepo msingi mpya wa ukuwaji wa muda mrefu wa uchumi na kwa taifa kutanzua mizozo ya kiuchumi ambayo waMarekani wamekua wakikabiliana nayo kwa miaka kadhaa sasa.

Bw Obama aliapa kuendelea kupigania mageuzi makubwa ya huduma za afya, akisema isipoidhinishwa na bunge gharama za bima zitaendelea kupanda na deni la Marekani litaendelea kuongezeka.

Alikiri kwamba nchi inakabiliwa na changamoto chungu nzima na kwamba baadhi ya maamuzi yake hayajaungwa mkono kisiasa na wengi. Ukosefu wa ajira Marekani umefikia asilimia 10. Nakisi ya bajeti imefikia matrilioni ya dola, na kiwango cha kukubaliana na kazi ya Obama kimeshuka tangu alipochukua madaraka mwaka mmoja uliopita.

Akitoa jibu la Republican, Gavana mpya wa Virginia Bob McDonnell alisema serekali kuu inajaribu kufanya mambo mengi mno na matokeo yake ni kuongeza deni la taifa kwa vizazi vijavyo.

Rais Obama alitoa mwito wa kusitisha matumizi ya serekali kuu kwa miaka mitatu kuanzia 2011 katika juhudi za kupunguza deni la taifa.

XS
SM
MD
LG