Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 03:05

Dunia yaungana kuisaida Haiti


Waandishi wa habari wiki hii walizungumzia habari kuu, huku kipaumbele kikiwa ule mkasa wa tetemeko la ardhi lililotokea Haiti siku ya Jumanne.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Atlanta BMJ Mureithi alieleza kuwa vyombo vya Marekani vilitoa muda wake mwingi kuelezea janga hilo ambapo watu wanaokisiwa kuwa zaidi ya elfu 50 wamepoteza maisha yao. Mureithi alisema Rais wa Marekani Barack Obama aliongoza juhudi za jamii ya kimataifa kusaidia raia wa Haiti kwa hali na Mali.

Kutoka Kenya, mwandishi wa habari wa gazeti la Daily Nation Douglas Mutua, alielezea utata unaoendelea kumkumba waziri Mkuu bwana Raila Odinga anayeongoza juhudi za kupanda miche katika msitu wa Mau leo siku ya Ijumaa. Mutua alieleza kuwa Rais Mwai Kibaki alitazamiwa kushirikiana na bwana Odinga katika shughuli hiyo lakini ametoa sababu za kutokwenda kwenye msitu huo.

Baadhi ya wanasiasa wa mkoa wa Rift Valley wamehamaki kutokana na juhudi za bwana Odinga za kuhifadhi msitu huo baada ya wakazi haramu kutoka mkoa huo kufukuzwa kwenye msitu wa Mau.

XS
SM
MD
LG