Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Januari 13, 2025 Local time: 00:17

Burundi: FNL yapongeza hatua ya serekali


Wizara ya mambo ya ndani ya Burundi ilitangaza Jumatano Januari 6 kwamba inatambua rasmi uwongozi wa sasa wa chama cha FNL. Uwamuzi huo umepongezwa na kiongozi wa FNL, Bw Agathon Rwasa alipozungumza na Sauti ya Amerika akisema, ni hatua inayobidi kuzingatiwa ili kuepusha watu wanaojaribu kusababisha vurugu nani ya vyama vya kisiasa.

Chama cha FNL klichokua kundi la mwisho la waasi kutia saini makubaliano ya amani ya Burundi 2006, kilikabiliwa na mvutano wa ndani kati ya Bw Rwasa na wafuasi wa msemaji mkuu wa chama Pasteur Habiymana. Wanachama hao walitaka kumondowa Rwasa kutoka uwongozi wa chama, lakini mkutano mkuu wa chama ulipooitishwa mwezi Novemba 2009 wanachama waloasi walifukuzwa kutoka chama kufuatana na Bw Rwasa.

Bw Rwasa amesema hivi sasa chama chake kinajitayarisha kushiriki katika uchaguzi mkuu unatoazamiwa kufanyika mnamo miezi minne ijayo. Hata hivyo kiongozi huyo amesema vyama vya upinzani havijaridhika na matayarisho ya uchaguzi huo, kutokana na matatizo mengi ambayo hayajatanzuliwa kabla ya uchaguzi.

Miongoni mwa matatizo hayo anasema una watu wengi ambao wamefika umri wa kupiga kura, miaka 18 hawajapata vitambulisho vyao, ambavyo vitahitajika wakati wa uchaguzi. Kiongozi wa FNL anasema inaonekana kana kwamba chama tawala cha CNDD-FDD kinapanga njama za kuiba kura, lakini matumaini yake ni kwamba masuala hayo yatatanzuliwa na uchaguzi utafanyika kwa njia ya haki.

XS
SM
MD
LG