Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 17:55

Kielelezo cha Katiba Kenya Kujadiliwa


Rasimu ya katiba mpya ya Kenya imechapishwa rasmi leo baada ya kamati ya wataalamu wa sheria kutoka nchini Kenya, Zambia, Afrika kusini na Uganda kuwasilisha kielelezo cha katiba mpya.

Kulingana na wataalamu hao wa sheria wananchi wa Kenya watapewa muda wa siku 30 kuisoma katiba hiyo na kuijadili na hatimaye kutoa maoni yao kuhusu mabadiliko yanayostahili kwenye kielelezo hicho cha katiba.

Kulingana na kielelezo hicho cha katiba Rais atapunguziwa mamlaka yake nchini Kenya na Waziri Mkuu atakuwa na uwezo wa kuunda serikali na pia kuteuwa baraza la mawaziri. Kulingana na mapendekezo hayo Rais atachaguliwa na wananchi na atakuwa Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya Kenya.

Mwenyekiti wa kamati ya wataalamu wa sheria Nzamba Kitonga anasema kwamba raia wa Kenya wasifikirie kuwa rais amepokonywa uwezo na mamlaka yake kwenye mapendekezo ya katiba mpya.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG