Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 02:55

Kabila atafuta suluhisho kwa Zimbabwe


Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Joseph Kabila, yupo mjini Harare kwa mazungumzo yenye lengo la kutatua mgogoro katika serikali tete ya umoja nchini Zimbabwe.Bwana kabila anakutana kwa mazungumzo Jumatatu na Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na waziri mkuu Morgan Tsvangirai.

Bwana Tsvangirai na chama chake cha MDC kiliahirisha kufanya kazi na bwana Mugabe na chama chake cha ZANU-PF hapo Octoba 16. Chama cha MDC kinasema ZANU-PF kinajaribu kuyumbisha mkataba wa kushirikiana madaraka uliotiwa saini mwaka jana kwa kufanya kampeni za kuwakamata na kuwadhalilisha maafisa wa MDC.

Bwana Kabila anatembelea Harare kama mwenyekiti wa jumuia ya maendeleo kusini mwa Afrika-SADC. Maafisa walisema Jumatatu kuwa viongozi watatu wa SADC watafanya mkutano siku ya Alhamisi, kwa matumaini ya kutatua matatizo yanayoendelea nchini Zimbabwe.

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unaahirisha kutoa msaada kwa baadhi ya vitengo vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, ikisema kuwa wamewauwa zaidi ya raia 60 mwaka huu.

Mkuu wa masuala ya kulinda usalama wa Umoja wa Mataifa Alain Le Roy alitangaza hatua hiyo Jumatatu, katika mahojiano na radio Okapi, inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa. Le Roy alisema wachunguzi wa Umoja wa Mataifa waligundua kwamba wanachama wa jeshi la Congo waliwauwa raia 62 kati ya mwezi Mei na September, katika kijiji cha Lukweli, kilichopo kaskazini-mashariki ya Goma.

XS
SM
MD
LG