Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 22:08

Washington yaongoza sherehe za siku ya makazi duniani


Sherehe za kimataifa kuadhimisha siku ya makazi duniani zimefanyika mjini Washington zikisimamiwa kwa ushirikiano kati ya wizara ya makazi na mipango ya miji ya Marekani na Idara ya makazi ya Umoja wa Mataifa UN-HABITAT.

Mada ya mwaka huu ni "Tupange Mustakbali wa Miji Yetu", katika lengo la kusisitiza umuhimu na haja ya haraka kukidhi mahitaji ya wakazi wa miji katika dunia inayoshuhudia ukuwaji wa haraka wa miji.

Katika ujumbe wake kuadhimisha siku hii ya Jumatatu ya kwanza ya kila mwezi wa Oktoba, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema changa moto kuu za miji kwa karne hiui ya 21 ni pamoja na ukuwaji wa haraka sana wa miji mingi na kupunguka kwa mingine, kupanuka kwa biashara zisizo rasmi na jukumu la miji mikuu katika kuchochea mabadiliko ya hali ya hewa.

Bw Ban alisema mipango ndiyo msingi wa ajenda hii , lakini mipango haiwezi kufanikiwa bila ya utawala bora, na wakazi maskini wa miji kulazimika kuchukua mamuzi yatakayoathiri maisha yao.

Mkurugenzi mkuu wa UN_HABITAT, Dk Anna Tibaijuka amesema kufanyika kwa sherehe za kimatiafa mjini Washingotn kutaleta kishinikizo kwa dunia nzima kuona jini taifa kuu la dunia pia linajishughulisha na hili suala la makazi kwa wote na ukuwaji wa miji.

XS
SM
MD
LG