Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 19:23

Uganda yamkamata afisa wa juu wa LRA


Jeshi la Uganda linasema limemkamata kamanda wa juu wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army na kukomboa watu 98 ambao walitekwa na waasi hao.

Msemaji wa jeshi la Uganda Luteni Kanali Felix Kulaigye, ameiambia Sauti ya Amerika kwamba jeshi limemkamata kamanda wa juu wa LRA Okot Atiak wakati wa operesheni ya hivi karibuni katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. alisema Kiongozi wa kundi hilo la LRA alikuwepo katika kambi hiyo hiyo lakini aliweza kukimbia.

Majeshi ya Uganda yalingia Jamhuri ya Afrika ya Kati, katika wiki za hivi kartibuni kutokana na kibali cha serekali ya nchi hiyo ili kuwasaka wapiganaji wa kundi hilo.

Atiak ana mahusiano ya karibu na kiongozi wa kundi hilo la waasi Joseph Kony na pia inasemekana alihusika katika mauaji ya 1995 ya watu zaidi ya 200 katika kijiji cha Atiak huko Uganda.

XS
SM
MD
LG