Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 21, 2024 Local time: 17:03

Africa inaweza kujitegemea amesema Clinton



Akihutubia kikao cha ufunguzi cha Mkutano wa AGOA huko Nairobi Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton amesema bara la Afrika linaweza kujitegemea kimaendeleo, akitoa mfano wa Rwanda. Amesema licha ya nchi hiyo kukabiliwa na vita na matatizo ya kikabila wananchi wa Rwanda hivi sasa wanajiamini wenyewe na viongozi wao wakiongozwa na Rais Paul Kagame..

"Wananchi wa Rwanda waliamini sera zinazotegemea ushahidi na matokeo yanayoweza kupimwa kuweza kujiendeleza katika maisha yao"

Bi Clinton alizungumzia juu ya umuhimu wa teknolojia ili kuimarisha biashara na maendeleo. Akizungumzia jinsi wafanyabiashara wa Afrika wanavyoweza kufaidika na mkonga mpya wa baharini unaojulikana kama "fiber optic" unaozunguka bara la Afrika ili kurahisisha mawasiliano ya simu na mtandao.

Amesema mfumo huu mpya utawasaidia wafanyabiashara na wananchi wa Afriika kuwasiliana na kufanya biashara na jamii ya Kimataifa.

Baada ya kuhutubia mkutano huo wa mawaziri wa biashara na viwanda kutoka nchi mbali mbali za Afrika zinazoshiriki katika mpango wa biashara nafua na Marekani AGOA, Bi Clinton alikutana na Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga juu ya masuala mbali mbali hasa matatizo ya kisiasa nchini humo.

Akizungumza na waandishi habari baada ya mazungumzo yake alieleza masikitiko yake kutokana na uamuzi wa viongozi wa nchi hiyo kutounda mahakama maalum ya kusikiliza kesi za wanaotuhumiwa kuhusika na ghasia za uchaguzi mapema mwaka jana.

Waziri huyo alisema kukosekana kwa taasisi thabiti na zenye nguvu nchini Kenya, kumeruhusu ulaji rushwa, kutohukumiwa watu, ghasia zenye uchochezi wa kisiasa, ukiukaji haki za binadamu na ukosefu wa heshima kwa utawala wa sheria.



XS
SM
MD
LG