Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 05:06

Serikali ya Kenya haitounda mahakama maalum


Serikali ya Kenya imetangaza Alhamisi jioni kwamba haitounda mahakama kusikiliza kesi za wanaotuhumiwa kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mapema mwaka 2008.

Baada ya kukutana kwa mara tatu kujadili suala hilo Baraza la Mawaziri lilikubaliana kwamba watuhumiwa watalazimika kufikishwa mbele ya Tume ya Ukweli na Maridhiano iliyoundwa hivi karibuni na Rais Mwai Kibaki kusikiliza kesi zao.

Kutokana na uamuzi huo taarifa ya serikali inaeleza kwamba watuhumiwa hao hawatafikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC huko The Hague kama ilivyo pendekezwa na mpatanishi mkuu wa mzozo wa kisiasa wa Kenya, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Matifa Bw Koffi Annan.

XS
SM
MD
LG