Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 18:33

Jeshi la DRC lakabiliana na waasi wa FDLR.


Jeshi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo limewafukuza waasi wa kundi la FDLR la Rwanda kwenye vijiji kadhaa katika mtaa wa Mwenge huko Kivu Kusini.

Zoezi hili linafuatia operesheni maalumu ya kijeshi iliyoanzishwa jana na jeshi la Congo, wakisaidiwa na kikosi cha kulinda amani cha Umoja Mataifa-MONUC.

Kamanda wa operesheni za kijeshi katika jimbo la Kivu Kusini, kanali Delifee Kaimbi ameiambia sauti ya Amerikakuwa wanajeshi wa Congo hivi sasa wamedhibiti miji ya Kigogo na Kitanda ambayo iliwahi kuwa ngome ya waasi wa FDLR.

Kanali Kaimbi amesema waasi hao wa FDLR hivi sasa wamekimbilia eneo jingine huko huko Kivu Kusini, lakini majeshi ya serikali yanaendelea na msako mkali dhidi ya waasi hao.

XS
SM
MD
LG