Rais Barack Obama amesema mataifa yenye viwanda vikuu na yale yanayoendelea yamefikia maridhiano ya kihistoria juu ya haja ya kuchukuliwa hatua za haraka kukabiliana na kuongezeka kwa hali ya joto duniani.
Rais wa Marekani alisema viongozi wa mataiga 17 walokutana huko L'Aquila, Italy walichukua hatua muhimu kabisa katika kutayarisha mkutano wa kimataifa wa mwezi wa Disemba huko Copenhagan juu ya namna ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Bw Obama alisema washiriki wa mkutano walikubali kwamba mataifa yenye viwanda lazima waongoze katika juhudi hizi na kuyasaidia mataifa yanayoendelea kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
waziri mkuu wa Australia Kevin Rudd alisema wajumbe walikubaliana kuundwa Taasisi ya Kimataifa ya Kunasa na kuhifadhi, itakayo kua na makao makuu yake nchini mwake ili kuratibu juhudi hizo zote.