Kwa mujibu wa BAKWATA kikubwa wanachokitaa waislam ni kujumuisha sheria za kislam kwenye sheria za nchi.
Katika tamko lake juu ya kuundwa kwa mahakama ya kadhi lililotolewa bungeni, waziri wa sheria na katiba alisema tume iliyoundwa kushughulikia suala la kuwepo au kutokuwepo kwa mahakama ya kadhi imetaka kutafsiriwa baadhi ya sheria za kislam na kuzijumuisha katika sheria za nchi na sio kuundwa kwa mahakama ya ki-islamu.
Sheikh mkuu wa Tanzania Issa bin Shaban Simba, katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar-es-salaam Alhamisi terhe 2 Julai alisema, “waziri anasema amekutana na wataalam hatujui wataalam wale ni wataalam wa sheria za kislam au ni wataalam wa kawaida".
Aliendelea kusisitiza kwamba “isione kigegezi serikali kuanzisha mahakama ya kadhi nchi hii ina mahakama mengi, mahakama ya nyumba kuna mahakama ya kadhi kuna mahakama za bahari za sheria wala hatudai kwamba kuna siku waislam katika mahakama hizo watakata mkono mtu au wataua mtu kesi za jinai ni kesi za mahakama kuu ya serikali” .
Sheikh Shaban Simba anasema kwa upande wao cha muhimu ni kutaka kuhukumu masuala ya ndoa na mirathi mambo ambayo anasema yanapotoshwa kwa muda mrefu.
Sheikh mkuu alisema “waziri hakufafanua ni nani atasimamia nani tunalozungumza si sheria ya kislam kuwepo lakini nani msimamizi wa sheria hizo. Tumechoshwa waislam kupotoshwa mambo yetu”.
Kwa mantiki hiyo Sheikh mkuu wa Tanzania alisema baraza kuu la waislam wa Tanzania linapinga hatua hiyo.