Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 03, 2025 Local time: 05:35

Misaada ya Benki ya Dunia Yazidi


Benki ya Dunia inasema imetoa kiasi cha dolla billioni 58.8 ambacho kinaweka rekodi ya misaada duniani kwa mwaka wa fedha wa 2009 kusaidia nchi zinazopambana na hali mbaya ya uchumi. Benki ya Dunia ilisema Jumatano fedha zilizotolewa kwa mwaka huu ni ongezeko la asilimia 54 kulinganisha na misaada iliyotolewa mwaka wa fedha uliopita.

Rais wa Benki ya Dunia Robert Zoellick anasema maombi ya misaada yaliongezeka vikubwa mwaka huu. Alisema maombi hayo huenda yakaendelea mwaka ujao, kwa sababu kasi ya kuboreka kwa hali ya uchumi haina uhakika. Watu katika mataifa masikini wameathirika zaidi na kuanguka kwa uchumi duniani.

Kupambana na mgogoro huo, Benki ya Dunia ilihimiza nchi zilizoendelea kutenga kiwango maalum katika matumizi yao ya kuchochea uchumi kwa ajili ya misaada kwa nchi za nje. Benki hiyo inasema wafadhili wameongeza michango yao kwa dolla billioni 6.8 kusaidia mipango ya kufufua uchumi.

XS
SM
MD
LG