Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 09:31

Serikali ya Mseto Kenya Hatarini Kusambaratika?


Hali ya kisiasa nchini Kenya inazidi kuwa ya wasiwasi mkubwa baada ya viongozi na wafuasi wa vyama vikuu vya siasa, ODM na PNU kushindwa kukubaliana kuhusu maswala nyeti yanayozusha uhasama nachuki Kati ya Rais Mwai Kibaki n Waziri Mkuu Raila Odinga.

Mgogoro wa sasa unahusisha nafasi ya kiongozi wa shughuli za serikali katika bunge ambayo kwa sasa inashikiliwa na Makamu wa Rais Kalonzo Musyoka ambaye aliteuliwa kushika nafasi hiyo na Rais Kibaki.

Lakini Bwana Odinga anadai kuwa nafasi hiyo inastahili kuchukuliwa na waziri mkuu na siyo makamu wa rais kwa maelezo kuwa hawezi kuwa waziri mkuu nje ya bunge, lakini ndani ya bunge ni mtu mwingine anaongoza.

Rais Barack Obama wa Marekani amewaandikia barua Rais Mwai Kibaki na Waziri Mkuu Raila Odinga akiwataka kushirikiana ili kuzuwia uwezekano wa ghasia na machafuko kama yale yaliyofuatia uchanguzi wa rais nchini humo mwaka 2007.

Tayari Waziri Mkuu Odinga ametangaza wazi kuwa suluhisho pekee ni kurudi mwenye uchanguzi kwa maelezo kuwa wamesukumbwa vya kutosha.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG