Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 30, 2024 Local time: 20:04

Ziara ya Rais Obama Nje ya Nchi


Hatua ya Rais Barack Obama wa Marekakani kupeana mikono na Rais Hugo Chavez wa Venezuela ilizua mjadala mkubwa miongoni mwa wanasiasa wa Marekani, baadhi wakiunga mkono na wengine wakisema kuwa yeye kama rais wa Marekani hakutakiwa kusalimiana na kiongozi wa nchi ambayo haina uhusiano mzuri na Marekani.

Lakini mchambuzi wa siasa Profesa Charles Bwenge wa chuo kikuu cha Florida Marekani, anasema shutuma dhidi ya Rais Obama ni za kisiasa na kwamba hazina msingi kwa manufaa ya taifa la Marekani.

Profesa Bwenge alisema kuwa shutuma hizo zinatoka kwa wapinzani ambao bado mawazo yao yamezingirwa katika karne ya 20, na ambao wako tayari kukosoa kila kitu kinachofanywa na Rais Obama.

Aidha Profesa Bwenge alisema watu hao bado wanaishi wakati wa vita baridi na hawako tayari kwa mabadiliko ambayo wakati wa kampeni za uchaguzi, Obama aliahidi kuyaleta kama akichaguliwa kwa rais wa Marekani.

Zinazohusiana

XS
SM
MD
LG