Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 06:36

Clinton Aionya Sudan na Washirika Wake


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema rais wa Sudan Omar El-Bashir atawajibika kwa vifo vyovyote vya wakimbizi huko Darfur kutokana na uamuzi wake wa kuyafukuza makundi ya kigeni yanayotoa msaada. Clinton anasema utawala wa Obama karibuni utamtaja mjumbe maalum kwa Sudan.

Akizungumza na waandishi wa habari katika afisi za wizara ya mambo ya nje bi Clinton aliyaonya pia mataifa yanayounga mkono hatua ya Bashir kuwa lazima wawe tayari kutoa huduma muhimu na wafanyikazi wa kuchukua nafasi za wale waliofukuza na bwana Bashir ili kudumisha na kuokoa maisha ya watu wasio na hatia huko Darfur.

Onyo ya waziri Clinton inaashiria maneno makali zaidi kutoka kwa afisa wa juu wa Marekani kuhusu uamuzi wa rais Bashir kuyafukuza makundi 13 ya misaada na kuyataka mashirika mengine yanayotoa huduma sawa kukomesha operesheni zao nchini Sudan ifikapo mwisho wa mwaka huu.


XS
SM
MD
LG