Waasi wa CNDP katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanasema wakotayari kufanya mazungumzo ya amani na serikali ya rais Joseph Kabila.
Maelezo hayo ya waasi wanaoongozwa na Jenerali Laurenti Nkuda yamekuja muda mfupi baada ya serikali ya nchi hiyo kusema kuwa mazungumzo ya moja kwa moja na waasi wa CNDP yatafanyika Nairobi Kenya.
Hatahivyo mkuu wa masuala ya kijamii wa CNDP dokta Alex Kasanzu amesema bado hawajapokea mwaliko rasmi wa mkutano huo, lakini anasema wako tayari kwa mazungumzo hayo.
Aidha dokta Kasanzu anasema pande zote husika zinatakiwa kufungua njia za mawasiliano kurahisisha kazi hiyo na kuleta matumaini kwa wananchi kuwa sasa ni wakati wa kutafuta amani ya nchi hiyo kwa njia za amani na siyo vita.