Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 27, 2024 Local time: 03:09

Siku ya Ukimwi Duniani


Siku ya ukimwi duniani Disemba mosi mwaka huu iliadhimishwa ikiwa ni miaka 20 tangu kutangazwa siku hiyo na Umoja wa Mataifa. Hapa Washington rais George Bush alisema, hadi kufikia mwisho wa mwaka huu mpango wake wa kupambana na ukimwi umefikia lengo lake la kutoa matibabu kwa watu milioni mbili wanaoishi Afrika.

Na ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imesema kupima mapena na kutoa matibabu kutaweza kuongeza sana matumaini ya kuishi watoto wachanga waloambukizwa na virusi vya HIV vinavyosababisha ukimwi. ripoti inaeleza kwamba kiwango cha kuishi kinafikia asili mia 75 kwa watoto walopimwa na kutibiwa mnamo wiki 12 za mwanzo za kuzaliwa kwao.

Huko Kenya mwito wa mwaka huu ni kuwataka watu wajipime mapema ili kujua ikiwa wameambukizwa au la, na kuzungumzia kwa uwazi matatizo ya ugonjwa huo.

XS
SM
MD
LG