Umoja wa mataifa unasema pande hizo mbili zilishambuliana karibu na kambi ya watu walio yakimbia makazi yao, kilomita 15 kaskazini mwa mji wa Goma, baada ya waasi wa kitusi kupiga risasi hewani.
Jijini Nairobi, katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekaririwa akisema machafuko hayo yanaweza kulitumbukiza eneo zima. Marais Joseph Kabila wa Congo, Paul Kagame wa Rwanda, na viongozi wengine kadhaa wa Afrika wanashiriki.
Mjumbe mpya wa umoja wa mataifa nchini Congo aliyeteuliwa hivi karibuni, rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo pia anahudhulia mkutano huo.
Wakati huo huo, waasi wanaoongozwa na jenerali Laurent Nkunda wameiambia Sauti ya Amerika kuwa hawadhani kuwa mkutano huo utaweza kuzaa matunda kwa madai kuwa mgogoro huo ni wa wa-Congo, na utatatuliwa na wa-Congo wenyewe.