Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 02, 2025 Local time: 23:59

Hezbollah yathibitisha kifo cha kiongozi wake Nasrallah


(FILES) Ki0ngozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah akizungumza kwa hamasa wakati wa mkutano wa kidini kusini mwa Beirut, 22 Septemba 2006.
(FILES) Ki0ngozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah akizungumza kwa hamasa wakati wa mkutano wa kidini kusini mwa Beirut, 22 Septemba 2006.

Kundi la Hezbollah nchini Lebanon limethibitisha Jumamosi kifo cha Sayyed Hassan Nasrallah aliyeuliwa kutokana na shambulio la bomu lililofanywa na jeshi la Israel.

Katika taarifa yake kundi hilo limesema litaendelea na vita dhidi ya Israel katika "kuiunga mkono Gaza na Palestina, na kuilinda Lebanon na wakazi wake."

Israel ilitangaza mapema Jumamosi kwamba imemuua Nasrallah kutokana na shambulio la anga katika kitongoji cha kusini cha Beirut siku ya Ijumaa.

Taarifa hiyo imesema kwamba kiongozi huyo aliuliwa pamoja na kamanda wa kikosi cha kusini cha kundi hilo Ali Karki, pamoja na makamanda wengine.

Kituo cha televisheni cha Hezbollah, Al-Manar kilianza kutangaza aya za Quran baada ya kutangaza kifo cha Nasrallah.

Wizara ya Afya ya Lebanon imesema kwamba karibu watu sita waliuliwa na 91 kujeruhiwa kutokana na shambulio hilo la Ijumaa.

Uharibifu baada ya shambulio la anga la Israel kwenye kitongoji cha kusini mwa Beirut.
Uharibifu baada ya shambulio la anga la Israel kwenye kitongoji cha kusini mwa Beirut.

Televisheni ya Lebanon imekuwa ikonyesha uharibifu uliotokana na shambulio hilo huku moshi ukiwa umetanda angani kutoka kwenye majengo yaliyobomolewa kabisa na uchafu uliozagaa mitaani.

Vyanzo vya habari vya Israel vinasema Marekani iliarifiwa muda mfupi kabla ya shambulio la anga la Ijumaa lakini, Waziri wa Ulinzi Llyod Austin anasema Marekani haikupewa onyo la mapema na wala haikuhusika na mashambulio ya Israel huko Beirut.

Forum

XS
SM
MD
LG