Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, amewambia waandishi habari siku ya Jumapili alipotembelea mji wa Port Said, makao makuu ya muda ya serikali, kwamba kiwango cha mzozo ni cha kushtusha na kwamba hatua za kudhibiti ugomvi na kupunguza maafa miongoni mwa raia hazitoshi.
Tedros amesema "kulingana na takwimu zilizopo, ugomvi wa Sudan hadi hivi sasa umesababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 20, kumbuka hiyo ikiwa ni idadi ya chini, kuna watu milioni 10 wamelazimika kukimbia makazi yao na kubaki ndani ya nchi, huku milioni 2 wamelazimika kukimbilia nchi za jirani."
"Huu ni mzozo mkubwa wa watu kupoteza makazi yao kwa wakati huu dunaini. na kiwango cha hali ya dhadura ni cha kutisha, na hakuna hatua za kutosha zinazochukuliwa kuzuia vita," amesema mkuu wa WHO.
Tedros ametoa wito wa kusitishwa mara moja vita na kufikia makubaliano yatakayopelekea suluhisho la kudumu la kisiasa na anatoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuamka na kuisaidia Sudan.
Mkuu huyo aliwatembelea wagonjwa katika hospitali moja huko Port Said na kukutana na maafisa wa serikali alipokua ananza ziara ya siku mbili katika mji huo unaoshikiliwa na serikali baada ya kufukuzwa Khartoum na kikosi cha dharura cha Sudan RSF.
Kulingana na mashahidi walozungumza na shirika la habari la AFP, mamia ya watu walikimbilia vitongoji vya kaskazini mwa Khartoum Jumamosi kufuatia mapigano makali kati ya jeshi na kikosi cha dharura karibu na kambi muhimu ya kijeshi.
Forum