Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 15:17

Bandari ya usafirishaji mafuta ya Libya imeacha kufanya kazi kutokana na uhaba wa mafuta ghafi


Mabomba na sehemu ya upakiaji ya bandari ya mafuta ya Marsa al Hariga katika mji wa Tobruk
Mabomba na sehemu ya upakiaji ya bandari ya mafuta ya Marsa al Hariga katika mji wa Tobruk

Bandari ya usafirishaji ya mafuta ya Libya ya Hariga imeacha kufanya kazi kutokana na uhaba wa mafuta ghafi, wahandisi wawili katika kituo hicho waliliambia Reuters siku ya Jumamosi.

Wahandisi wawili katika kituo hicho waliambia Reuters siku ya Jumamosi, wakati mapigano kati ya makundi hasimu ya kisiasa yakisababisha kufungwa kwa maeneo mengi yenye utajiri wa mafuta nchini humo.

Kushambuliana kwa wiki hii katika mzozo unaohusu udhibiti wa benki kuu kunatishia kusababisha hali mpya ya kudorora kwa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini, mzalishaji mkuu wa mafuta ambayo imegawanyika kati ya pande za mashariki na magharibi.

Utawala wenye makao yake makuu mashariki, ambao unadhibiti maeneo ya mafuta ambayo yanachukua karibu uzalishaji wote wa nchi, unataka mamlaka za magharibi kuacha kutaka kuchukua nafasi ya gavana wa benki kuu nafasi muhimu katika nchi ambayo udhibiti wa mapato ya mafuta ni tuzo kubwa zaidi kwa makundi yote.

Forum

XS
SM
MD
LG