Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Agosti 24, 2024 Local time: 17:18

Wanajeshi 9 wa FARDC wauawa na wanamgambo magharibi mwa DRC


Picha ya maktaba: Wapigananaji wa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Picha ya maktaba: Wapigananaji wa Jamahuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maafisa wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamethibitishwa kwamba kundi la wanamgambo magharibi mwa nchi hiyo, liliwaua wanajeshi tisa katika kambi ya jeshi katika kijiji kimoja mwishoni mwa wiki.

Msemaji wa jeshi na chifu wa kijiji jirani walisema kuwa maafisa hao waliuawa katika jimbo ambalo limeshuhudia mapigano ya jamii mbalimbali, ya kuzozania ardhi tangu mwaka 2022.

Shambulio hilo lilitokea katika eneo la Kwamouth katika jimbo la Mai-Ndombe, ambapo jamii mbili hasimu - Wateke na Waka - zimekuwa zikipigania ardhi iliyo karibu na Mto Kongo.

Wanamgambo wengi wa Yaka wanaojulikana kama Mobondo walifanya shambulio katika kijiji cha Kinsele, karibu kilomita 130 kaskazini mashariki mwa mji mkuu, Kinshasa.

Msemaji wa jeshi la Kongo Sylvain Ekenge alisema washambuliaji 35 pia waliuawa.

Chifu wa kijiji cha jirani cha Kimomo alisema meja, luteni, makapteni wawili na wanajeshi watano waliuawa.

"Waliwafumania askari kwenye kituo chao mwendo wa saa 5 asubuhi," alisema Stanys Libye. "Jeshi lililipiza kisasi na baadhi ya washambuliaji walizidiwa nguvu."

Forum

XS
SM
MD
LG