Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 20:50

Mazungumzo ya amani ya kundi la Oromo na serikali ya Ethiopia yashindwa kuleta muafaka


Duru ya pili ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Ethiopia na kundi la waasi yenye lengo la kumaliza mzozo uliodumu kwa miongo kadhaa katika jimbo kubwa la Oromiya nchini humo yamemalizika bila makubaliano, pande zote mbili zilisema Jumanne.

Mazungumzo ya Tanzania kati ya serikali na Jeshi la Ukombozi la Oromo (OLA) yalifuatia mazungumzo ya Aprili na Mei ambayo pia hayakuweza kuleta makubaliano.

OLA ni kikundi kilichoharamishwa cha chama cha upinzani kilichokuwa kimepigwa marufuku ambacho kilirejea kutoka uhamishoni mwaka wa 2018.

Malalamiko yake yanatokana na madai ya kutengwa na kutelekezwa kwa watu wa Oromiya, wanaopatikana kando ya mji mkuu Addis Ababa.

Ghasia huko Oromiya zimesababisha vifo vya mamia ya watu katika miaka michache iliyopita, na mzozo huo umekua moja wapo ya matatizo makuu ya usalama yanayomkabili waziri mkuu Abiy Ahmed tangu kumalizika mwaka jana kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu miaka miwili katika jimbo la Tigray.

Forum

XS
SM
MD
LG