Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 23:49

UNESCO inataka kuhakikisha Kiswahili kinatamalaki mtandaoni


Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO .
Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO .

Dunia inapoadhimisha mwaka wa pili wa Siku ya Kiswahili, kauli mbiu ikiwa “kuibua uwezo wa Kiswahili katika enzi ya kidijitali,” mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema anataka kiswahili kitamalaki pia kwenye mitandao.

Akizungumza mjini Paris makao makuu ya UNESCO, BiAudrey Azoulay amesema “Kiswahili ni lugha inayozungumzwa na watu wa zamani na wa sasa. Ikiwa na wazungumzaji zaidi ya milioni 200, ni mojawapo ya lugha za Kiafrika zinazotumiwa sana, ikijumuisha lahaja zaidi ya kumi na mbili kuu. Kwa karne nyingi, lugha hii ya Kibantu imeibuka kama njia ya kawaida ya mawasiliano katika maeneo mengi ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, pamoja na Mashariki ya Kati.”

Ujumbe wa mkuu huyo wa UNESCO umeendelea kusema kwamba “Kiswahili hakisimulii tu hadithi ya mazungumzo kati ya lugha, bali pia mazungumzo kati ya watu na nchi. Kwa hakika, kwa sababu Kiswahili hushiriki maneno na dhana na lugha nyingine za Kiafrika, kina nguvu ya kuvutia ya kuunganisha watu.”

Sherehe za siku ya kiswahili zimefanyika katika nchi zote za Afrika Mashsariki na Kati na sehemu nyingine za dunia.

Tofauti na mwaka 2022 ambapo asasi mbalimbali za kielimu – hasa vyuo vikuu – zilifanya maadhimisho ya kwanza ya SIKIDU katika viwango vyao binafsi, serikali kuu mara hii zilikamata usukani wa maandalizi na zimekuwa mstari wa mbele kufanikisha mipango yote.

Viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wamekua wakitoa wito wa kuzihimiza nchi za Afrika kufundisha kiswahili pamoja na kulinda utamaduni, mila na desturi za waswahili .

Forum

XS
SM
MD
LG