Msemaji wa ubalozi wa China hapa Washington, Liu Pengyu ameieleza VOA kwamba China imeona maudhui muhimu kwenye azimio la Washington.
Ameongeza kusema kwamba tabia ya Marekani ni matokeo ya mtazamo wake kwa vita baridi, na kwamba kile Marekani inachokifanya kinasababisha uchokozi wa kikanda, kudhoofisha mifumo ya nyuklia isiyo na madhara, na kusumbua maslahi ya kimkakati na mataifa mengine.
Azimio la Washington ambalo rais wa Marekani, Joe Biden na rais wa Korea Kusini, Yoon Suk Yeol, wamelitoa Aprili 26, linajumuisha juhudi za kukabiliana na mashambulizi ya nyuklia kutoka Korea Kaskazini.
Washirika walikubaliana kuongeza sauti ya Seoul katika mipango ya nyuklia ya Marekani kupitia chombo maalumu.