Siku ya Jumatano, wakurugenzi wakuu wa benki ya bunia walichagua pendekezo la rais Biden, Ajay Banga, kuongoza taasisi hiyo.
Kiongozi huyo ambaye ni Mmarekani wa kuandikishwa aliyezaliwa India ni kiongozi wa zamani wa masuala ya mikopo.
“Ajay Banga, atakuwa kiongozi atakayeleta mabadiliko, kuleta utaalamu, na ubunifu katika nafasi yake kama rais wa benki ya dunia,” alisema rais Biden katika taarifa yake.
Rai wa sasa wa benki ya dunia David Malpass, alijiuzulu mwezi Febuari katikati ya kutolewa mwito wa kujiuzulu baada ya kutoa kauli zilizo ashiria kupuuzia masuala ya mabadiliko ya hali hewa.