Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 16:08

Sudan yadaiwa kusitisha mapigano licha ya mashambulizi kuendelea


Vikundi vya kijeshi vinavyopigana vya Sudan vilikubaliana Jumanne kwa usitishaji vita mpya wa wiki moja kuanzia Alhamisi, Sudan Kusini ilitangaza

Licha ya hayo mashambulizi zaidi ya anga na ufyatuaji risasi katika eneo la Khartoum yaliendelea na kuharibu makubaliano ya sasa ya kusimamisha mapigano.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, alisisitiza umuhimu wa kusitishwa mapigano na kutangaza majina ya wajumbe wa mazungumzo ya amani ambayo pande zote zimeridhia.

Lakini matokeo ya mwisho ya makubaliano ya kusitisha mapigano ya Mei 4 mpaka 11 kati ya mkuu wa jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Burhan, na Jenerali wa kikosi cha akiba Mohamed Hamdan Dagalo hayakuwa wazi kwa sababu ya ukiukwaji mkubwa uliovuruga makubaliano ya awali.

Mapigano ya sasa yakiwa katika wiki yake ya tatu yamewalazimu watu 100,000 kuikimbia Sudan.

XS
SM
MD
LG